- Nyumbani
- Utangulizi
Utangulizi
Tanzania ni maarufu kwa mamalia wakubwa katika mazingira ya aina mbalimbali. Wanyama kama tembo na simba wanawavutia watu wengi, lakini kuna aina nyingi sana za spishi za mamalia wadogo. Baadhi ya mamalia wadogo na wa pekee wanaishi Tanzania tu na wamo katika hatari kubwa ya kutoweka kabisa.
Tovuti hii imeandaliwa kwa ajili ya kuwaelimisha watu ambao siyo wataalamu wa mamalia wa Tanzania lakini wanavutiwa na viumbe hawa. Aidha tovuti hii imetayarishwa kwa ajili ya kuwasaidia wana biolojia wanaofanya utafiti juu ya mamalia wadogo na kujihusisha na uhifadhi wao.
Lengo kuu la tovuti hii ni kuwaelezea mamalia wote wa Tanzania, lakini mwanzoni tutaelezea spishi zinazopatikana kwenye milima ya Tanzania, nchi iliyopo Afrika Mashariki. Milima hii imegawanywa kwenye makundi manne makuu: milima ya kaskazini (ikijumuisha Kilimanjaro na Ngorongoro), Tao la Mashariki (ikijumuisha milima ya Usambara na Udzungwa), milima ya kusini (ikijumuisha Rungwe na Kitulo) na ufa wa Albertine (ikijumuisha Mahale). Kila kundi uasili tofauti wa kijiolojia na mifumo ya tabia ya nchi tofauti. Kuna,mamalia ambao wapo katika makundi haya yote ya milima na wengine wanapatikana kwenye kundi moja tu ya milima hii.
Tovuti hii ina taarifa zitakazokusaidia kuwatambua mamalia wa Tanzania, kuelezea kila spishi (kwa sasa tutaelezea spishi ambazo ziko kwenye kwenye maeneo yaliyopo mita 1,000 au zaidi kutoka usawa wa bahari au makundi mengine yatakayochaguliwa), muhtasari wa milima mbalimbali ya Tanzania na data zao, na vitu vitakavyotumika katika mipango ya elimu inayolenga mamalia wa Tanzania.
Tutafurahi sana kupata maoni na mapendekezo ya watu wote watakaotumia tovuti hii, ili tuweze kuiboresha. Mnaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia anwani ya barua pepe ifuatayo: MammalsofTanzania@fieldmuseum.org