- Nyumbani
- Maelekezo (Sw Skull Key Instructions)
Maelekezo (Sw Skull Key Instructions)
Wakati wa kutumia sifa bainifu, inabidi kuchagua taarifa sahihi kwenye kila hatua hadi unapofanikiwa kukitambua sawasawa kielelezo kilicho mbele yako.
ANZA MWANZONI KABISA MWA ZOEZI (isipokuwa kama unafahamu aina ya mamalia unayemchunguza).
Mtumiaji anapewa taarifa mbili zinazoambatana na picha iliyopo kwenye skrini (screen), taarifa hizi zinahusu sifa bainifu za kielelezo na inabidi achague taarifa zinazolingana na ngozi au fuu la mamalia anayehusika. Inabidi achague moja kati ya taarifa hizi mbili juu ya kielelezo kwani haiwezekani kwa zote mbili kuwa sahihi; moja tu ndio sahihi. Kwa mfano:
1A) Kuna meno kwenye fuu.
AU
1B) Hakuna meno kwenye fuu.
Unapochagua mojawapo ya taarifa, unaweza kubonyeza kwa kutumia “mouse” kwenye picha au alama sahihi kwenye skrini (screen).
Utakapochagua taarifa zinazolingana na kielelezo kinachohusika, utaona orodha nyingine ya taarifa na inabidi uchague tena taarifa zinazolingana na kielelezo. Hatimaye, taarifa unazochagua kwenye hatua mbalimbali zitakufikisha kwenye jenasi ya mamalia anayehusika, ambayo,inabainisha kwa usahihi kielelezo unachochunguza. Utapata jibu sahihi iwapo (a) taarifa na sifa bainifu zimetayarishwa vizuri na (b) umefuata hatua zote vizuri.
Unapotumia taarifa hizi kumbuka yafuatayo:
1) Picha zinazoonyeshwa zinahusu sehemu maalum za kielelezo. Wakati mwingine, kielelezo cha mkononi mwako hakifanani kabisa na kielelezo kinachoonyeshwa katika picha iliyopo kwenye skrini. Huenda saizi na muundo wa kielelezo chako ni tofauti na picha unayoona na huenda sehemu nyingine hailingani na unachoona kwenye picha. Haina maana kwamba chaguao lako ni kosa. Inabidi utazame sehemu ya kielelezo ambayo inaelezwa. Kwa mfano, iwapo fuu ambalo unataka kubainisha lina meno, chagua “1) Kuna meno kwenye fuu”, hata kama meno yaliyoko kwenye kielelezo hayafanani kabisa na meno yaliyoonyeshwa kwenye picha ya skrini.
2) Inabidi uwe mwangalifu kuhusu taarifa na sifa zinazotolewa katika maelezo. Kumbuka kwamba maelezo yanaweza yakaorodhesha vigezo kadhaa. Lazima kielelezo chako kilingane na vigezo VYOTE vilivyoorodheshwa. Kwa hiyo iwapo kigezo kimoja kinakosekana, ni,lazima uchague HAPANA.
Kwa mfano:
1A)
A) Mwili hauna nywele.
B) Masikio ni marefu na yamechongoka
C) Pua ni ndefu.
D) Kucha za miguu zina umbo la chepeo (spade shaped).
Bonyeza hapa. >>